Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya March 23 2016 usijali millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari nane kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10…Ahadi Ya Mamilioni Ya Rais Magufuli Vijijini
Baada ya kufunga kikao cha bodi ya Barabara Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amesema ‘Hizi pesa ni za mikopo lakini sahivi mnatakiwa kuangalia ni jinsi gani hizi pesa zitakuwa na matokeo gani katika Halmashauri zenu‘>>>Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Habari kutoka ITV...Wizi wa Mafuta Ya Ndege
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni Hamad Masauni amewasimamisha kazi watumishi waliokutwa na madumu 10 ya mafuta ya ndege wakiwa na gari ya Serikali,
‘Ukishachukua mafuta ya ndege alafu ndege inaanguka inauwa watu alafu kumbe wewe ni Askari wa zima moto au Askari Polisi sasa hawa nawaasimamisha kazi mara moja na hatu kali za kisheria zitafuata‘Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni Hamad Masauni
Habari kutoka ITV…Dawa Bandia Za Mimea
Wakaguzi wa viuatilifu wakamata shehena ya Dawa bandia za mimea Mlimbana na kukutwa na hatia ya kuajiri watoto wenye umri chini ya miaka 15.
‘Viuatilifu kama hivi kuviweka juani ni makosa makubwa sana alafu mtoto mdogo kama huyu kumuweke hapa kwa ajili ya kuuza sumu kama hii bila kinga sio vizuri>>>Wakaguzi
Habari kutoka Star TV…Kujiunganishia Umeme Kinyemelezi
Meneja wa Shirika la Umeme Mwanza Mwandisi Sara Aseyi amewaambia watu wanaojiusisha na kujiunganishia Umeme kinyume cha sheria waache mara moja kwani zoezi Hilo ni endelevu ‘Wateja wa Milimani nawaambia waache wizi mara moja‘ Mwandisi Sara Aseyi
Habari kuyoka Star TV…Tuhuma Za Uhalifu
Polisi Kilimanjaro washikilia Watu 24, kufuatia na tukio lilotokea jana saa tatu usiku maeneo ya kijiji cha Kombo Wilayani Moshi Vijijini
‘Mtu anayeitwa Linda Malisa alijeruhiwa kwa kupigwa na risasi sehemu ya mguu wa kulia kwenye ugoko na tumboni na Askari waliokuwepo kwenye oparesheni ya kuua Mbwa na katika msako huo wahamiaji 19 kutoa Ethiopia walikamatwa‘>>>ACP Wilbroard Mtafungwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.
Habari kutoka TBC1…Serikali Ya Zanzibar Yaombwa Kuwapa Kipaumbele Wazee Katika Afya
‘Tuseme tu kwamaba raia wote wa Zanzibar wako sawa wawe wa CCM, CUF na Vyama vingine na watapewa ulinzi sawasawa kabisa hakuna ubaguzi na hii hali ya doria ilihimarishwa tu kama tahadhari na tahadhari hii itapungua pale tutakapo hakikisha hakuna hali yeyote ya uhalifu‘>>>.Charles Kitwanga Waziri wa Mambo ya Ndani Ya Nchi
Habari kutoka TBC1...Waziri wa Nishati na Madini Apokea Taarifa ya Kamati Iliyochunguza Malalamiko
Waziri Muhongo ameyasema hayo baada ya kupata taarifa aliyoipata kutoka kwenye kamati alaiyoiunda kwa ajili ya kuchunguza malamiko ya wananchi wa nyamongo wanaouzunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara
‘Yaliyoko huku sio ya wana kamati yaliyoko huku wamekusanya maoni kutoka kwa Wananchi, wamiliki wa Migodi na kutoka kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali na hatakaye yakataa haya na sisi tuta mkataa‘>>>Prof: Sospeter Muhongo Waziri wa Nishati na Madini
Habari kutoka Azam TWO…Makonda: Hatutorejesha Baadhi ya Silaha
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema hawatarejesha baadhi ya silaha ‘Lakini kuna wengine wazazi wao wametangulia mbele za haki kwahiyo mimi sidhani kuwa kwenye Mirathi unaweza ukaandikiwa urithi silaha kama bunduki‘>>>Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE
KAMA ULIKOSA SENTENSI ZA WAZIRI WA AFYA KUHUSU WAZEE NA USUMBU HOSPITALI TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI…