Habari niliyoipokea muda mfupi uliopita zinamhusu Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Magembe kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori Charles Mulokozi kwa kutoa vibali vya kusafirisha wanyama kwenda nje pamoja na wakurugenzi wanne wa Huduma za misitu kutokana na usafirishaji na uvunaji holela wa magogo.
Akizungumza na kituo cha ITV Waziri Magembe amesema….>>>‘watu wanavuna mazao ya misitu kule kalambo, tukaenda kule tukakutana na magogo mengi sana yako msituni ambayo yanatakiwa yawe yamelipiwa na hayakulipiwa, nimewaondoa hili tuweke uongozi mpya kwa sababu kinachoonekana ni kwamba hawana uwezo wa kuongoza’
Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori Charles Mulokozi, Waziri Magembe amesema .…..>>>Jana usiku tumekamata ndege ambayo ilikuwa inasafirisha nyani, inaonekana ni biashara inayofanywa kwa hiyo amesimamishwa kazi, uchunguzi ufanywe ili tuone hili jambo la kusafirisha wanyama nje ya nchi limefanywa kiasi gani na ni nani anafanya’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
UNAPENDA MOVIE ZA KITANZANIA? KUNA HIKI KIPISI CHA MOVIE YA MATRON WA SHULE ALIYEMZIMIA MWANAFUNZI… TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
https://www.youtube.com/watch?v=bFp4y3bgu0U