Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine
Serikali imewasimamisha kazi watumishi 11 wa Wizara ya Maliasili na Utalii ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imewataka waajiri nchini, kuwapa kipaumbele wazawa pindi wanapotaka kuajiri wafanyakazi #MTANZANIA #March 25
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali 'PAC', imekusudia kuzihoji idara sita za Serikali juu ya kuongezeka kwa deni la Taifa #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Serikali Mkoani Tanga imeeleza kuwa kuzuiwa kwa Waziri wa Kenya kuingia Bandarini ni kutokana na kutokuwa na taarifa za ujio wake #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Shule za bweni zimetajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaougua Kifua Kikuu 'TB' kutokana na mazingira mabaya ya malazi #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Marekani, Ulaya wasusia mwaliko wa kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Z'bar, Dk. Ali Mohamed Shein #NIPASHE #March 25
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Marais wastaafu wa Tanzania wa awamu ya tatu na ya nne jana hawakuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Z'bar Dk Ali Mohammed Shein #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Manispaa ya K'ndoni na Temeke zimepokea bil 8 kwa ajili ya kuwakopesha vijana na wanawake ili kuendeleza biashara zao #NIPASHE #March 25
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri, watakiwa kuwasilisha orodha ya watumishi hewa ifikapo March 30, ili ikabidhiwe kwa Rais #UHURU
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Yanga, Azam FC zitalazimika kucheza mechi nne ndani ya siku 10 kutokana na TFF kuzipiga kalenda mara kwa mara mechi zao za Ligi Kuu #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) March 25, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
Uliikosa video ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alipokutana na Balozi wa China? Angalia video hii hapa chini