Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya March 25 2016 usijali millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Clouds TV…Makonda Aomba Baraka Za Mufti
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametumia siku hii ya Ijumaa Kuu kwenda kupata baraka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, ‘Nishauku yangu kufika kwa Mufti wangu ni kutambua ya kwamba hakuna mamlaka utakayoweza kuyapata nje ya mikono ya mungu‘.>>>Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Habari kutoka Channel 10…Wizi wa Maji Dar es salaam
Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es salaam Dawasco imewataka wakazi wa Mkoa huo kufata sheria na utarartibu uliowekwa na mamlaka hiyo. ‘Nachukua fursa hii kuwaomba kama unataka kusimamia biashara ya maji kwa niaba ya Dawasco, njoo Dawasco Magomeni‘>>>Meneja wa Dawasco
Habari kutoka Azam TWO…Wavuvi Walalamikia Kodi Ziwa Nyasa
Wavuvi wa Ziwa Nyasa wameliomba bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia marekebisho ya kodi ya uvuvi.’Ningeliomba Bunge la awamu ya tano lingejaribu kukaa na kutafakari kuhusiana na leseni za uvuvi hususani kwenye ziwa Nyasa‘>>>Mvuvi
Habari kutoka ITV…Ijumaa Kuu
Askofu msaidizi Dar es salaam amewataka wenye mamlaka kusimamia haki.’Naombeni sana wapendwa katika maisha na katika majukumu yetu mbalimbali tuwatendee watu haki, usawa na kwa wema‘>>> Askofu Msaidizi Dar
Habari kutoa Star TV...Ujenzi wa Taifa
Serikali ya shauriwa kushirikiana na viongozi wa dini amabapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amefika kwa aajili ya kujitambulisha kwa Mufti Mkuu wa Tanzania ili aweze kuongoza vizuri Dar es salaam.’Mh. Makonda aweze kuongoza vizuri kazi zake, na mkituunga mkono mwanzo wa mambo na sio kutuunga mkono mwishoni ili tuweze kutoa mchango wetu’>>>Mufti Mkuu wa Tanzania
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM
HAYA NDIO MAAMUZI YA RC MAKONDA YAMESABABISHA HII BARABARA KUFIKIA HAPA..