Mwaka 2012-2013 Serikali ya Tanzania ilikopa Dola za kimarekani milioni 600 (zaidi ya bilioni 13) kutoka benki ya Standard ya Uingereza kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa makubaliano ya kulipa deni hilo pamoja na riba ya 1.4% inasemekana katika mazingira yasiyojulikana fedha iliongezwa na kuwa 2.4%.
Kwa taarifa ya Serikali iliyotolewa na aliyekuwa katibu Mkuu Ombeni Sefue siku kadhaa zilizopita alieleza kuwa katika mkopo huo hawakuhitaji wakala lakini mwaka 2013 iligundulika kuwa fedha Taslimu Dola milioni 6 ziliingizwa katika akaunti ya kampuni ya Egma ambayo mwenyekiti wake ni aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya.
April 01 2016 Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania, Shose Sinare wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kutokana na makosa yanayowakabili, watuhumiwa wamenyimwa dhamani na kesi yao itasomwa tena April 8 2016.
Uliikosa video ya wabunge watatu walivyofikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa? Angalia video hii hapa chini
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE