Moja ya vitu ambavyo najua mtu wangu ulitamani kuvijua baada ya uchaguzi wa marudio Zanzibar uliosusiwa na baadhi ya vyama vya siasa ni hatma ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.
April 05 2016 Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakati akilihutubia Baraza la Wawakilishi katika ufunguzi wa baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dr Shein amesema hakutakuwa na Serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio kushindwa kutimiza matakwa ya kikatiba hivyo serikali itaundwa na Serikali moja pekee, Dk. Shein amesema…
>>>‘kwa kuzingatia msingi huo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha katiba cha 36(43) hakuna chama cha siasa ambacho kinakidhi masharti ya kustahiki kutoa makamu wa kwanza wa Rais, suala la kulinda na kudumisha muungano wetu wa Serikali mbili kwangu halina mbadala nitaendelea na juhudi za kudumisha Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar‘:- Dk. Shein
Ayo Tv ilipata nafasi ya kuzungumza na Mwanasheria Jebra Kambole kuhusu uwezekano wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, Mwanasheria huyo aliyazungumza haya…..
>>>’Makamu wa Rais atakuwa ni mtu yule ambaye ametoka chama ambacho kimepata 10% kwenda juu ya kura za urais, lakini ibara hiyo ya 39 imetoa mwongozo kwamba endapo hakuna chama ambacho kimefikisha 10% au mgombea wa urais halikuwa hana mpinzani wa aina yoyote, katiba hiyo inatoa mwongozo katika ibara ya 39(3) inasema kwamba chama cha upinzani chenye uwakilishi mwingi ndio kina uwezo wa kutoa makamu wa Rais’:-Kambole
>>>’katiba hiyo inatoa mwongozo kwamba chama cha upinzani ambacho kitakuwa na sifa hizo kitatuma jina kwenda kwa Rais ndani ya siku saba toka Rais amepata madaraka na rais atamteua mtu huyo lakini zikipita siku saba hiyo nafasi itaachwa wazi’:-Kambole
ULIIKOSA YA KAMA KUNA UWEZEKANO WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZNZ? MTAZAME HUYU MWANASHERIA HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE