Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) chini ya Umoja wa Mataifa limekuwa likitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa takribani miaka mitatu. Siku kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kulituhumu jeshi hilo kuhusika na unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa kwa wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
April 08 2016 kutoka makao makuu ya Jeshi hilo wametoa taarifa za kusikitishwa na tuhuma hizo na hapa Afisa Habari wa Jeshi hilo James Macheta, ameyazungumza haya….>>>’Jeshi letu haliwezi kupuuza taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukua hatua za kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu ya ulinzi wa amani zilizokwishafanywa na jeshi letu zinaonyesha hakukuwa na tuhuma kama hizo’.
UNAWEZA KUANGALIA TAARIFA NZIMA ILIYOTOKA MAKAO MAKUU YA JWTZ KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI…
ULIKOSA MAAMUZI YA RAIS MAGUFULI KWA MKUU WA MAJESHI MWAMUNYANGE? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE