Kama wewe ni mpenzi wa kufuatilia kinachoendelea katika taarifa za habari kupitia TV za Tanzania na ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya April 14 2016 usijali millardayo.com inakupatia fursa ya kuziangalia Habari sita kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10…Mapambano ya Kurushiana Risasi
Polisi Mkoani Shinyanga wamewaua Majambazi 3 na kufanikiwa kukamata bunduki mbili aina ya SMG pamoja na Pikipiki aina ya San Lg , ‘wakati wote tunatakiwa kuwa tayari na wananchi wamefurahi ni jinsi gani tumewahi najua kuna wengine walikuwa hawako kazini lakini wamejitahidi wamekuja>>>Askari Polisi
Habari kutoka TBC1…Asilimia 71 ya Watanzania Hawana Utamaduni wa Kufanya Kazi Zinazochangia Pato la Taifa
‘Sheria Takwimu namba tisa ya mwaka 2015 takwimu hizi sasa ndio rasmi ndio takwimu za kutathmini kufuatilia sera zetu ya kazi na ajira na tayari takwimu hizi jinsi tunavyozungumza tuko ofisini tukiangalia namna ya kutumia takwimuhizi’>>>Dk. Alibina Chuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Habari kutoka TBC1…Takukuru Yabaini Watumishi Hewa Watano Ambao Majina Yao Hayakuwasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa
‘Halmashauri nyingine ambazo tunaelekea tunapoendelea na ili zoezi wawe waangalifu sana na makini kama mtu hayupo ni bora uweke wazi maana Serikali inatumia hela nyingi kuwalipa watumishi hewa>>>Henry Makare Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mwanza
Habari kutoka Star TV…Ubadhirifu Fedha za Pembejeo
Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameyanena haya ‘Afisa Mtendaji na Wajumbe wote wapembejeo, OCD wakamate kuanzia sasa hivi wachukulie maelezo wenye kesi peleka Mahakamani wakapate haki yao, amri ya pili Mkurugenzi naomba umfute kazi Afisa Mtendaji‘>>>Glorious Luoga Mkuu wa Wilaya ya Tarime
Habari kutoka Star TV…Watumishi Jijini Mwanza, Mkurugenzi, Afisa Utumishi lawamani
‘Tayari tumebaini kuna uongo ambao unakwenda kwenye hizi Halmashauri kwamaana ya kwamba orodha ya majina yaliyoorodheshwa kwa Mkuu wa Mkoa haina majina yote kwamaana tumefanya uchunguzi, tunaamini Halmashauri ya Jiji la Mwanza wanawatambua’>>>Mhandisi Ernest Makale Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza.
Habari kutoka Azam TWO..Mabenki Yanatakiwa Kuwafuatilia Wakopaji
Waziri wa Ardhi Nyumba maendeleo na Makazi William Lukuvi amezitaka taasisi za kibenki kufuatilia mikopo wanayoitoa kwa ajili ya kuendeleza sekta ya Ardhi ‘nitafurahi sana hizi taasisi za kibenki badala ya kutumia hizi pesa , waweze kuwakopesha na kuweza kuongeza kipato kwa wananchi‘>>>Waziri Lukuvi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard AyokwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE
ULIKOSA MAELEZO YA DAKIKA 5 YA MJOMBA AKIELEZEA DAKIKA ZA MWISHO KABLA NDANDA KOSOVO HAJAFARIKI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI