Leo April 16 2016 Rais John Pombe Magufuli amefanya uzinduzi wa barabara ya juu ‘Flyover’ Dar es salaam, barabara inayotarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2018.
Lengo likiwa ni kupunguza kero za usafiri katika jijila Dar es salaam, Barabara ambayo inatengenezwa chini ya usimamizi wa Serikali ya Japani, Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amesema ‘Kuna watu wakati tukibuni hili jambo walianza kuleta maneno na kusema ni jambo lisilowezekana, na sasa kazi imeanza na itawezekana, nataka tuifanye Tanzania kama Ulaya‘
‘Imefika wakati shughuli nyingi zinaharibika kwa sababu ya foleni, hata baadhi ya ndoa sasa zinavunjika kwa sababu watu wanachelewa kurudi majumbani kwao, sasa kwa huu mradi wa barabara za juu nahakika utatatua matatizo yote‘
‘Niwakumbushetu ndugu zangu, uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa kuwatumikia watanzania, tuweke uchama na usiasa pembeni na tusimame kwa pamoja maendeleo ya watanzania‘
Pia Rais Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika harakati zake za kuhakikisha Dar es salaam inakuwa safi ‘Nimpongeze sana mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa project yake aliyoianzisha katika kuifanya Dar es salaam kuwa safi, niwambeni tumuunge mkono‘
‘Ni aibu unamkuta mtu anatupa ovyo takataka,tena mwingine hata eneo laketu la nyumbani anashindwa kusafisha, hii haipendezi yhata kidogo‘;-Rais Magufuli
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE