Chaguzi za Meya wa Jiji la Dar es salaam ziliahirishwa mara tatu na baadaye akapatikana Diwani wa Kata ya Vijibweni, Temeke Isaya Mwita ‘Chadema’ kuwa shauku kubwa ilihamia kwenye kumjua atakayekuwa naibu wake.
April 21 2016 umefanyika uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam ambapo wajumbe 16 kati 18 walifika kwa ajili kushiriki uchaguzi huo. Matokeo ya uchaguzi yalimpa ushindi Diwani wa kata ya Kiwalani Musa Kafana ‘CUF’ ambapo alishinda kwa kura 10 na kumshinda mpinzani wake Diwani wa kata ya Mchafukoge Mariam Mohamed ‘CCM‘ aliyepata kura 6.
Kwa matokeo hayo Mussa Kafana ‘CUF’ ndiye amekuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam
ULIIKOSA DAKIKA 11 ZA VURUGU ZILIVYOTOKEA KATIKA UCHAGUZI WA MEYA DA ES SALAAM? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE