Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Tanzania (CAG) Profesa Juma Musa Asaad ameamua kuweka wazi mambo kadhaa kuhusiana na ripoti yake, kikubwa alichozungumza mkaguzi mkuu kabla ya kuamini ripoti yoyote inayoandikwa mitandaoni, unatakiwa uangalie vitu viwili muhimu ili kufahama kama hiyo ni ripoti yake au la.
Ripoti inayotoka kwa CAG huwa ina vitu viwili muhimu vya kuzingatia ili uweze kujiridhisha na kufahamu, ripoti ya CAG ni lazima iwe na saini au kama itatolewa moja moja huwa ina muhuri wa kuthibitisha kuwa hiyo ni ripoti ya CAG. Hivyo ndio vitu viwili muhimu ambavyo vinaweza kukudhihirishia kuwa hii ni ripoti rasm ya CAG.
“Kwa sababu unataka taarifa rasmi hivi ni vitu vya kuzingatia kuhusu ripoti yangu, ripoti yangu tofauti yake ni kwamba inakuwa na saini na pia ripoti zetu kama ikitoka moja moja inakuwa na muhuri wa kuthibitisha kuwa hii ni ripoti rasmi”
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
SPIKA WA BUNGE HAKUIKALIA KIMYA KAULI YA HUYU MBUNGE