Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo May 4 2016 kwa klabu ya Azam FC kucheza mchezo wake wa 27 wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya JKT Ruvu na kubakisha michezo mitatu ya Ligi ili kuweza kumaliza msimu wa 2015/2016.
Azam FC wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex Mbande Chamazi, wamelazimishwa sare ya goli 2-2 na JKT Ruvu ambayo kabla ya mchezo huo ilikuwa nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu, yaani ipo katika nafasi ya timu tatu za Ligi zinazoweza kushuka daraja mwisho wa msimu.
Mchezo ulikuwa mwepesi kwa Azam FC ambao awali walianza kufunga magoli mawili dakika ya 31 kupitia kwa Michael Balou baadae dakika ya 37 Kipre Tchetche akafanikiwa kufunga goli la pili kwa Azam FC, wakati JKT Ruvu walianza kusawazisha magoli yote mawili kuanzia dakika ya 56 kupitia kwa Saady Kipanga na dakika ya 72 kupitia kwa Mussa Juma.
Kwa matokeo hayo Azam FC sasa inakuwa kama imejiondoa katika mbio za kuipiku Yanga katika nafasi ya kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu bara msimu wa 2015/2016, kwa sasa Azam FC na Yanga watakuwa wamepishana point 8, lakini kila mmoja ana mechi tatu, Yanga wakishinda mechi yao inayofuata rasmi watakuwa Mabingwa wa Ligi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: AZAM FC VS ESPERANCE (FULL TIME 2-1) APRIL 10 2016
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c