Bunge la Uingereza May 4 ilikuwa kama kuna vichekesho baada ya mjadala kuzuka ndani ya bunge hilo kutokana na mmoja kati ya wabunge kuuliza swali kwa waziri mkuu wa Uingereza, wakati wa muda wa maswali na majibu kuhusu mtangazaji wa BBC Gary Lineker kutotimiza ahadi yake.
Gary Lineker aliwahi kuhaidi kuwa kama Leicester City itafanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza, basi atafanya TV show yake akiwa na nguo ya ndani pekee, kitendo ambacho bado hajakitekeleza, mbunge Keith Vaz ambaye ni shabiki mkubwa wa Leicester aliingia bungeni na Scarf ya Leicester na wakati wa maswali na majibu alimuuliza swali waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Keith Vaz alihoji kuhusu ahadi ya mtangazaji huyo wa BBC Gary Lineker ambaye amewahi kuichezea Leicester City miaka ya nyuma katika nafasi ya ushambuliaji, kuwa alihaidi kufanya Tv show yake akiwa na nguo ya ndani, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alimjibu na kumwambia Lineker anastahili kutekeleza ahadi yake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: AZAM FC VS ESPERANCE (FULL TIME 2-1) APRIL 10 2016
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c