Mei 8 2016 ni siku ya wakinamama Duniani, Tanzania pia imekuwa moja ya nchi iliyofanya maadhimisho hayo, Hapa nakukutanisha na Makamu wa Rais Samia Suluhu ambaye leo alikuwa Dodoma na baada ya kuhutubia wananchi wake akaguswa na hili la kodi kwa wafanyabiashara wanawake na kutoa maamuzi..
‘Mimi kama mama nachukizwa na jambo moja kubwa nililoliona kule Moshi na baaadhi ya maeneo kule Arusha, kuna kodi zinatolewa katika masoko, Ukipita masoko ya Moshi na Arusha Unakuta wakinamama wanasimama na ndizi kichwani anasimama na ndizi yake hadi aiuze’
‘Na akiiweka chini anatozwa kodi na kodi ile ni sawa na bei anayoiuza. Kwahiyo mama anabakia na ndizi yake kichwni mpaka aiuze.’
‘Naelekeza Wakurugenzi wa halmashauri kufuta kodi hiyo mara moja, na nitafanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa jambo hili. Na siotu kodi za ndizi bali kodi zote zinazowazalilissha wakinamama’
ULIIKOSA HII YA TUNDU LISSU KAWASILISHA MAONI HAYA KUHUSU SERIKALI YA RAIS MAGUFULI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE