Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda aliwaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe.
Leo May 09 2016 katika uchunguzi wa awamu ya tatu wamekuja na ripoti ya watumishi hewa 74 walioisababishia Serikali hasara ya BILIONI 3.636 ambapo idadi ya watumishi hewa kwa mkoa wa Dar es salaam inafikia 283.
Paul Makonda amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Manispaa ya Ilala, Francis Kilawe kwa tuhuma za kuwaficha watumishi hewa 11 ambao walikuwa hawajulikani wapo idara gani.
#Breaking Mkuu wa Mkoa Dar, Makonda amemsimamisha kazi afisa utumishi Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11 pic.twitter.com/bU9tSP6giu
— millardayo (@millardayo) May 9, 2016
YAMEKUPITA MAGAZETI YA MAY 09 2016? KUTANA NA MREMBO ALICE KWENYE UCHAMBUZI WA MAGAZETI, UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE