Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo May 13 2016 limetangaza kwa mara ya kwanza katibu mkuu mwanamke katika historia ya shirikisho hilo, FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal kuwa katibu mkuu wa kwanza wa shirikisho la hilo mwanamke.
Fatma Samba Diouf Samoura anaingia FIFA mwezi June kuanza kazi rasmi na kurithi nafasi ya Jerome Valcke katibu mkuu wa shirikisho hilo aliyefungiwa miaka 12 kutokujihusisha na soka, Samoura mwenye miaka 54 ametangazwa leo katika mkutano uliofanyika Mexico.
FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura ambaye CV yake inaonesha kuwa amewahi kufanya kazi katika umoja wa mataifa UN kwa miaka 21, mabadiliko hayo yamefanyika ikiwa ni muendelezo wa mabadiliko katika shirikisho hilo, baada ya Rais wa zamani wa shirikisho hilo Sepp Blatter kuachia ngazi.
KASEJA KAZUNGUMZIA GOLI ALILOFUNGWA NA TAMBWE MAY 10 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE