Nchi ya India ni moja ya nchi katika bara la Asia ambapo wiki hii wamezichukua headline kwa kuvunja rekodi ya kuwa na joto kali zaidi ambalo limefikia hadi sentigredi 51 huko mjini Phalodi magharibi mwa Rajasthan. Mji huu ambao ni jangwa liitwalo Thar limechangia pia kuwa na pepo zitokazo magharibi zikiwa na hali ya umoto.
Joto hili limepelekea kufa kwa mifugo na mazao kuharibika na kuacha watu milioni 330 wakiwa na shida ya maji kutokana na ukame huo, pia janga hili limewapata mji wa Guru ambapo joto lao limefika sentigredi 50 kwa tofauti ya asilimia moja tu, New Delhi nao wamefikisha takribani sentigredi 47.
Rekodi zinasema hali hii ilishawapata India kwenye mji wa Alwar hukohuko Rajasthan baada ya kufikisha sentigredi 50.6 mnamo mwaka 1959.
ULIKOSA HII YA AGNESS MARWA KUSIMAMA TENA BUNGENI NA KUZUNGUMZA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE