Wateja wapatao milioni 11 wa Vodacom Tanzania wanaotumia huduma ya M-Pesa kuanzia leo wataanza kupatiwa mgao wa bonasi kutoka kwenye fungu la shilingi bilioni 25 zilizohifadhiwa kwenye akaunti maalumu ya M-Pesa kwenye mabenki mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao amesema……>>> “Mgao wa fedha hizi kwa wateja wetu ni mwendelezo wa kugawa fedha za bonasi ya M-pesa ambao ni utaratibu wetu. Hapo awali tuligawa takriban bilioni 20; awamu hii inayoanza leo tutagawa bilioni 25 na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa gawio kila baada ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Ferrao.
‘kiasi cha fedha atakachopata mteja kwenye mgao wa fedha hizi utategemea matumizi yake ya huduma hii katika kufanya miamala mbalimbali ya malipo ikiwemo kutuma fedha’;- Ian Ferrao
‘Natoa wito kwa wateja wetu ambao wameacha kutumia kadi zetu za simu wakati waliwahi kutumia huduma hii wajiunganishe tena kwenye mtandao wetu ili fedha za mgao wao zisipotee bure’;-Ian Ferrao
‘Pia wateja wetu wanaotumia huduma hii kuanzia leo wanaweza kuangalia fedha watakazojipatia kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kuandika neno KIASI na kuutuma kwenda namba 15300’-Ian Ferrao
Ferrao ameongeza kuwa wateja wa huduma ya M-Pesa wakiwemo mawakala wakubwa na wadogo wanao uhuru wa kutumia fedha zao za mgao watakazopata ambapo wanaweza kuzitumia kununulia huduma mbalimbali za Vodacom kama muda wa maongezi, kujiunga na vipurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha DABO BANDO.
ULIKOSA HII YA MAFIKIZOLO WALYOWASILI TANZANIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE