Matukio ya ndege yameendelea kutokea mwaka huu, Egypt Air May 19 2016 ilianguka na kuua abiria wote, leo May 27 ndege ya Korean air aina ya Boeing 777 imepasuka injini moja ya kushoto na kuwaka moto dakika chache kabla ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Haneda Tokyo kuelekea Seoul.
Taarifa zilizotolewa na Japan Television zinasema ndege hiyo iliyokua na abiria 307 na Wafanyakazi 17 walihamishwa kwa haraka kwenye ndege hiyo lakini bado moto huo uliwajeruhi watu 7 wakiwemo wanaume wawili na wanawake watano.
Magari mawili ya zima moto yalifika eneo la tukio na kuzima moto huo ambapo chanzo cha hitilafu ya ndege hiyo bado hakijajulikana na uchunguzi bado unaendelea.
https://www.youtube.com/watch?v=ZlVH0lE-ZSI
UNAFAHAMU WASIFU ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WILSON KABWE? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE