Ishu za wanafunzi vyuoni kufukuzwa na migomo zimezidi kuchukua headlines ambapo baada ya UDOM na UDSM, taarifa niliyoipata ni kutokea Kilombero, Ifakara kwenye chuo kikuu kishiriki cha tiba na afya cha St. Fransis.
Taarifa hiyo inasema wanafunzi wapatao 134 wa mwaka wa tatu wa shahada ya udaktari 134 hawajaingia madarasani kwa takribani wiki kadhaa ambapo mmoja wa wanafunzi hao amezungumza na millardayo.com na kueleza haya madai baada ya kasoro mbalimbali kujitokeza kwenye matokeo yao ya muhula wa tano……
>>>Utawala umesema haya mambo yatawezekana lakini kwa sababu utawala wamekuwa na ahadi nyingi hewa wanafunzi tumeona ili tuweze kuendelea na masomo inabidi tujiridhishe na matokeo yetu ya mwisho ya muhula wa tano kama yako vizuri ili tuendelee na muhula wa sita na hapo mvutano ndio ukaanza.
Unaweza kumsikiliza kwa kubonyeza play hapa chini
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Achilles Ndege amekuja na majibu kuhusu madai hayo………
>>>shughuli yao haijahitimishwa kutakuwa na mkutano mwingine wa bodi June 17 kwangu itakuwa mapema kulizungumzia, sababu iliyowafanya wasiudhurie darasani ni ya kinidhamu zaidi kuliko ya kitaaluma, walikataa kuingia darasani, walikataaa kufanya mtihani waliandamana kwa hiyo walitishia maisha ya wenzao, hoja zao zinashughulikiwa walikuwa na hoja za msingi.
Unaweza kumsikiliza kwa kubonyeza play hapa chini
ULIKOSA HUU UFAFANUZI WA WAZIRI NDALICHAKO KUHUSU KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI UDOM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI