Serikali imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotoka kila wiki lililodai kuwa Rais John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.
Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa “Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively”
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa amesema……
>>>”Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma”
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi meneja uhusiano wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda amesema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli
Ameongeza kuwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.
Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.
ULIKOSA HII YA FREEMAN MBOWE KUHUSU UPINZANI KUTOLEWA TENA BUNGENI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE