Mkurugenzi wa mashtaka ‘DPP’ alikata Rufaa mahakama kuu ya Tanzania akipinga uamuzi wa kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha.
Uamuzi uliotolewa na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na hakimu mkazi Emillius Mchauru kwenye kesi inayowakabili Kamishna Mkuu wa zamani wa TRA Harry Kitilya, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon.
June 09 2016 Mahakama ya Rufani imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es salaam iliyotupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kupinga kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili.
Hukumu hiyo imesomwa leo mahakamani hapo na Msajili wa mahakama hiyo, Zahra Maluma ambapo alisema mbali ya kutenguliwa kwa uamuzi huo pia Mahakama Kuu imeamriwa kusikiliza rufani ya msingi ya DPP.
Msajili Maluma alibainisha kuwa hatua hiyo inatokana na jopo la majaji kupitia uamuzi wa Mahakama Kuu na kubaini kwamba Jaji Moses Mzuna alikosea kutoa uamuzi uliosema kuwa kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha katika kesi inayomkabili Kitilya na wenzake hakutamaliza wala kuathiri shauri hilo.
ULIKOSA HAYA YA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU KUHUSU RUFANI YA KITILYA NA WENZAKE? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE