Wanasema imani ya mtu ndio ukombozi wake, ikiashiria kama utaamini basi utapona. Zipo nchi ambazo huaminika katika maswala ya matibabu India pia ikiwemo, ila matibabu haya ya kuwamezesha samaki walio hai watoto pamoja na watu wenye matatizo ya kifua yamewashangaza wengi.
Huu umekuwa utamaduni wao wa muda mrefu huku wakiamini kuwa njia hii inaweza kurahisisha upumuaji kwa watoto na pia kwa wagonjwa wa Pumu hii ndio tiba sahihi. Kila June familia mbalimbali hujumuika kwa pamoja ili kushiriki katika zoezi hili.
Mdomoni mwa samaki hao wanaweka dawa za asili zenye rangi ya njano na kuhakikisha anayepokea anameza vyote. Zoezi hili limekuwa likifanyika kwa miaka 170 ikiwa mwaka huu inakadiriwa zaidi ya watu laki moja walipokea tiba hiyo.
ILIKUPITA, UFAFANUZI UMETOLEWA KUHUSU MTI UNAODAIWA KUTOKELEZEA SURA YA MWL NYERERE>>>
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE