Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Mdami alisema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa ambapo katika hatua ya kwanza mamlaka hiyo inachakata taarifa za wananchi walizotoa wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga Kura kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Utoaji wa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji umeelezwa kuwa utasaidia kuwatambua wahusika pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii……>>>“Upatikanaji wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma”
Utoaji huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za utambulisho kwa wananchi ili zisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati mchakato wa kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.
Mdami alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili ya uhakiki wa taarifa hizo. Lengo la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba mwaka huu wananchi wote wawe wamepatiwa namba ya utambulisho .
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUMSIMAMISHA JKAZI BOSI WA NIDA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE