June 14 2016 Mwenyekiti wa chama cha TLP na mbunge wa zamani wa jimbo la vunjo Agustino Mrema amekutana na vyombo vya habari nakuzungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama vya upinzani kutomhukumu Rais Magufuli kwa sababu hana nia ya kuua upinzani kama wanavyodai.
Mbele ya waandishi wa habari Mrema amesema wapinzani ndio waliokubuhu katika kuvunja haki za binadamu, sheria katiba na demokrasia, kama walivyomfanyia na kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo la Vunjo.
Hizi ni sentensi za mrema……>>>‘kwanza ninachotaka kusema ni kwamba nataka kuonyesha wapinzani si wazuri kama wanavyotaka Taifa liwaamini si wakweli na wananchi wawe macho sana wasifikiri kila mpinzani ni mkweli wanayoyafanya ni haya lazima tuyafichue lazima yasemwe waziwazi‘
>>>’kwahiyo mimi ninachotaka kusema ni kwamba wala sisemi haya kwa sababu ya kutaka kufukua makaburi, nataka watu wajue kwamba wapinzani vitendo wanavyovifanya sio vya haki na hawamtendei haki Rais, wampe nafasi aongoze nchi hii wasimsingizie vitu vingi’
>>>Mimi ni mpinzani lakini nitaendelea kuwasema wapinzani ambao hawana deomokrasia, hawazingatii haki za binadamu wala hawazingatii katiba, sheria na ni mafisadi mimi nitawasema, uwe CCM mimi nitakusema, uwe upinzani nitakusema, wala siogopi wala sitaacha mimi sio CCM, mimi ni mpinzani, mzalendo na mkweli‘
ULIKOSA HII YA ZITTO KABWE KUHUSU KONGAMANO LA BAJETI NA YEYE KUSAKWA NA POLISI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE