Kwa kawaida wanyama wakali kama Simba, Chui, na wengine huwekwa chini ya usimamizi mkali endapo kukiwa na hatari ya kudhuru binadamu ama wanyama wanaowazunguka. Ila taarifa za kuwahukumu simba watatu kifungo cha maisha baada ya kugundulika wamemla mtoto wa miaka 14 huko India kimeshangaza wengi
Kwa kawaida tumezoea kuona Simba akiuliwa kama ikitokea kamshambulia binadamu lakini sio kufungwa, ila India wamefikia maamuzi tofauti kidogo ya kuwafungia kifungo cha maisha Simba watatu kutokana na wananchi wa eneo hilo kulalamika kutokea kwa matukio hayo.
Simba hao watatu, wawili wakiwa wakike na dume mmoja, walimshambulia mtoto aliyekuwa amelala nje ya nyumba kwenye bustani katika hifadhi ya taifa ya Gir Gujarat India. Mtoto huyo atakuwa mtu wa tatu kuliwa na Simba tangu April 2016 hali ambayo ilisababisha wananchi wa eneo hilo kuiomba serikali ichukue hatua ili kutokomeza matukio ya aina hiyo.
ULIKOSA KILICHOMCHEKESHA RAIS MAGUFULI JAPO ALIKUA KAVAA SURA YA KAZI IKULU? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE