Mitandao ya kijamii imekua ikirahisisha mfumo mzima wa upatikanaji wa habari pia swala zima la sayansi na teknolojia. Pamoja na faida zake hizo bado kuna madhara ambayo yanasababishwa na matumizi ya mitandao hiyo ya kijamii. Hali ambayo imepeleka serikali ya Algeria kusitisha matumizi ya mitandao ya kijamii kwa sasa.
Hii imetokana na kuwepo kwa udanganyifu wakati wa mitihani ambapo wanafunzi walibainika kutumia mitandao ya kijamii kuvujisha mitihani. Hivyo serikali imewalazimu kutotumia mitandao ya kijamii kwa kipindi hichi ambacho wanafunzi wa sekondari wanafanya mitihani ya kuhitimu ili kujiunga na elimu ya juu.
Uvujishaji wa mitihani kupitia mitandao ya kijamii umekuwa tatizo kwa muda sasa nchini humo. Serikali inaamini kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza matukio kama hayo.
DAKIKA 30 ZA MTANZANIA HALLEN ALIYETAJWA FORBES KUWA BILIONEA AJAE
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE