Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo kuanzia leo June 23, 2016 ili kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kusimamia vizuri maiti wakati wa kuzitoa kwa ndugu mara mbili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa na Hospitali kwa ujumla.
Prof. Museru amemteua Dkt.Flora Lwakatare Mkuu wa idara ya Radiolojia kukaimu nafasi hiyo.Kurugenzi ya Tiba Shirikishi inasimamia idara ya mionzi na idara ya Maabara ambapo kitengo cha kuhifadhi maiti kipo chini maabara.Vilevile Prof. Museru ametengua uteuzi wa Mkuu wa kitengo cha kuhifahi maiti Hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Innocent Mosha na kumteua Dkt Herbert Nguvumali kukaimu nafasi hiyo.
ULIIKOSA HII YA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUWAHUDUMIA WAGONJWA WA MOYO BURE BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE