June 28 2016 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti la mawio kwenye habari yenye kichwa kinachosema ‘Zanzibar Machafuko yaja’ dhidi yake na wenzake watatu.
Nje ya mahakama hiyo Lissu alizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa kauli ambayo imewafanya polisi wamuite kwa ajili ya mahojiano, Lissu alisema….
>>>’nchi yetu inaingizwa kwenye giza nene na dikteta uchwara hatuwezi kuongozwa na mtu wa namna hiyo, hata kama kachaguliwa na kuwa Rais‘
Lissu alifika kituo kikuu cha polisi Dar es salaam kuitikia wito wa polisi na amehojiwa na polisi kwa masaa matatu kutokana na kauli hiyo atalala rumande leo kwa amri ya ZCO baada ya kukosa dhamana na atafikishwa mahakamani kesho.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA HII YA TUNDU LISSU KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA UCHOCHEZI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE