Bado headlines za mechi kati ya Dar es Salaam Young Africans dhidi ya TP Mazembe iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0 inazidi kuchukua headlines, kutokana na kitendo cha Yanga kuamua mechi hiyo mashabiki waingie bure uwanjani.
Kitendo hicho cha Yanga ambacho kinatajwa kuhatarisha maisha ya mashabiki waliojitokeza na miundombinu ya uwanja, shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kupitia Rais wake Jamal Malinzi kuwa, kuanzia sasa mechi zote za kimataifa hazitoratibiwa tena na vilabu, kitendo ambacho kinatafsiriwa kama hakutatokea tena mashabiki kuruhusiwa kuingia bure uwanjani.
“Nimewaita kutokana na hali isio ya kawaida iliyojitokeza katika mchezo kati ya Yanga na TP Mazembe, TFF ndio chombo chenye mamlaka ya kuratibu michuano ya ndani na kimataifa yanayohusisha timu za Tanzania, kutokana na kitendo walichofanya Yanga, TFF imeamua kuwa itakuwa inaratibu mechi zote na sio tena vilabu”
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE