Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ilifungua kesi ya madai ya fidia ya Sh. bilioni 500 Mahakama kuu, kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Zitto Kabwe. IPTL pamoja na wadai wenzake waliiomba mahakama imwamuru Zitto kulipa fidia hiyo kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kimaandishi
Kesi hiyo dhidi ya Zitto Kabwe na gazeti la Raia Mwema leo imeahirishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania mpaka August 24 2016 baada ya mawakili wa IPTL kusema shahidi wao muhimu ameumwa ghafla hivyo hataweza kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo IPTL na mmiliki wake wanadai walipwe Tshs 500,000,000 (Bilioni mia tano) kwa madai kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika uongo dhidi ya IPTL kuhusu hela zilizoibiwa kwenye Escrow Akaunti.
ULIKOSA HUU UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 04 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE