Mwaka 2014 ndio Tanzania ililetewa taarifa za kwamba Benki kuu ya Tanzania inaileta sarafu ya shilingi mia tano hivyo ile noti ya shilingi mia tano inaondolewa kwenye mzungumko.
Mtaalamu wa fedha kutoka benki kuu ya Tanzania Patrick Fata amekaa kwenye Exclusive ya AyoTV na kusema yafuatayo kuhusu maendeleo ya sarafu ya shilingi mia tano >>> ‘Mzunguko wa sarafu ya shilingi mia tano sasa hivi unakwenda vizuri’
‘Nia yetu sisi tulivyotengeneza hii safaru ya 500 sababu ile noti ilitumika kama chenchi na inazunguka sana, ile noti ya shilingi mia tano tuliitengeneza ili iishi kwa miezi saba tu lakini badala yake ikawa hairudi mpaka miaka minne hadi mitano hivyo inachakaa haraka tofauti na elfu 10‘
‘Noti ya elfu kumi mtu akiipata anaipeleka benki lakini ile noti ya 500 unanunua soda, mtu wa mkaa ataitumia, Mama Ntilie nae ataisambaza na itazunguka hata hairudi benki kuu’
‘Hiyo ndio sababu tukaamua kutoa sarafu ya shilingi 500 ambapo inaweza kudumu miaka 15, 20 mpaka 30 na itaepusha gharama kwa serikali kuchapisha noti tena‘ – Patrick
Full story ya Patrick akiongea iko hapa kwenye hii video hapa chini..
EXCLUSIVE: UMEIKOSA YA WEMA SEPETU KUHUSU DIAMOND KUMPOST INSTAGRAM JUZI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI