Kesi ya Kikatiba ya namba 5 ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na Rebeca Gyumi, mwanaharakati wa haki za binadamu hasa haki za mtoto wakike na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la ‘Msichana Initiative’ linalofanya kazi ya kutetea haki ya mtoto wa kike kupata elimu ambapo kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Dar es salaam.
AyoTV imempata wakili wa Rebeca Gyumi wakili Jebra Kambole ambapo ameeleza kuwa mahakama imefikia maamuzi ya kutoa amri kwa Serikali kubadili sheria ya ndoa hususani katika vifungu ambavyo vinaruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa kwa sababu ni sheria kandamizi.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA HUU MPANGO WA NYUMBA ZA DAR ES SALAAM KUWA NA MABOMBA YA GESI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI