Baada ya July 7 2016 kamati ya maadili kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro, leo July 8 2016 kupitia kwa afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas ametoa msimamo wa TFF ambao walikuwa wamemshitaki Jerry na Mabrouk katika kamati ya maadili.
Alfred Lucas ambaye ameeleza msimamo wa katibu wa TFF Selestine Mwesigwa kuhusiana na kutoridhishwa na hukumu ya Mabrouk lakini ya Jerry Muro licha ya kutokutwa na hatia ya kosa moja kati ya matatu, TFF wameridhika na adhabu ya Jerry ila wanajiandaa kukata rufaa ya Naseeb Mabrouk.
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1