Habari inayotrend kwa sasa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa ni hii ya mke wa Donald Trump kudaiwa kuchukua maneno ya hotuba ya mke wa Rais wa Barack Obama, hotuba hiyo ya Melania inadaiwa kuwa na maandishi yaliyotolewa kutoka kwenye hotuba ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle, aliyoitoa miaka minane iliyopita.
Mke wa Trump amesema alipata usaidizi mdogo sana wakati wa kuandika hotuba hiyo, ambayo imesisitiza sana maadili ya kifamilia na kujumuishwa kwa watu wa matabaka yote.
Sehemu moja ya hotuba ya mke wa Trump inasema ……..>>>’Wazazi wangu walinifunza umuhimu wa kutia bidii kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako ndilo linaweka uhusiano na unafaa kutenda unachosema na kutimiza ahadi kwamba lazima uwaheshimu watu’.
Hotuba ya mke wa Obama mwaka 2008 ilisema: ……>>>’Mimi na Barack tulilelewa na maadili karibu sawa, kwamba unatia bidii kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako linaweka uhusiano na kwamba unafaa kutenda unachosema utatenda; kwamba lazima uwaheshimu watu, hata kama huwafahamu, na hata kama haukubaliani nao‘.
https://www.youtube.com/watch?v=hKc9GT7HEz4
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JULY 19 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI