Mwanzoni mwa mwaka 2016 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu, Rebeca Gyumi kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocates, walipinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.
July 08 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivi vya sheria ya ndoa vinapingana na katiba ya nchi kwa kuweka umri tofauti wa kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Mahakama pia iliitaka serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele hivi tata ndani ya mwaka mmoja.
Kwenye interview hii na Ayo TV na millardayo.com, Rebeca Gyumi ameelezea mpango wao baada ya kushinda kesi hiyo……>>>’tuna mpango wa kukaa na kuangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kuwahusisha wadau wote muhimu ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii, kwa sababu ni muhimu sana kwa jamii kuweza kuelewa athari ya ndoa za utotoni’.
>>>’Mpango uliopo ni kuielimisha jamii ielewe sheria hii inamaanisha nini na pili kuelimisha athari za kuoza watoto wakiwa wadogo na vilevile kuhamasisha kuwekeza zaidi kwa mtoto wa kike kumpatia elimu ili na yeye aweze kutimiza ndoto zake’
ULIKOSA HII YA REBECA GYUMI KUSHINDA KESI YA KUPINGA NDOA KATIKA UMRI MDOGO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI