Baada ya kuwepo kwa taarifa za watanzania kukamatwa wakienda kujiunga na vikundi vya kigaidi na hazikupatikana taarifa zozote za kuthibitisha hilo.
Sasa leo July 20 2016 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi, Augustine Mahiga, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za Afrika uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda, pia ameligusia suala la ugaidi.
Waziri Mahiga amesema ……..>>>’aliniambia pale airport, huyu ni kamishna kwamba ili tatizo ningependa mlijue vijana wenu wengi wengine wamekamatwa na wengine wameuawa pale Somalia hivyo hili tatizo tulitafutie mkakati ili mlielewe zaidi kwa hiyo aliniambia hivyo‘
ULIKOSA HII YA WAZIRI MAHIGA KUZUNGUMZIA PASSPORT YA AFRIKA ILIYOZINDULIWA HIVI KARIBUNI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI