Leo July 21 2016 Bunge la Afrika mashariki limekaa kikao cha dharura na kuitaka nchi ya burundi kumalizia mgogoro wa kisiasa uliopo hii ni baada ya kuuawa kwa risasi kwa aliyekuwa mbunge wa bunge hilo Hafsa Mossi.
Hafsa Mossi alikuwa ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi aliuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura, Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Akizungumza baada ya kikao hicho Spika wa bunge la Afrika Mashariki, Daniel Kidega amesema….. >>> ‘tumeketi kama bunge tuongee na kuonyesha upendo wetu kwa yeye kama mbunge mwenzetu na vilevile kuiambia serikali ya Burundi na serikali yote ya Afrika Mashariki wajaribu sana kutafuta amani’
ULIIKOSA HII YA WATANZANIA KUUAWA NA WENGINE KUKAMATWA WAKIWA NA AL SHABAAB? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI