Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo July 28 2016 mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.
Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo July 28 2016. Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Uteuzi wa Joseph Odo Haule umeanza leo July 28 2016. Kabla ya uteuzi huo Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund). Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
ULIKOSA SABABU ZA RAIS MAGUFULI KUHAMIA DODOMA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI