Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 29 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza na wananchi wa Manyoni Singida Rais Magufuli amezungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge na mahakama ya ufisadi ambapo amesema ……>>> ‘hawakuingia kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke’
ULIKOSA HII YA MAGUFULI KUHUSU MADAI YA KUZUIA SHUGHULI ZA KISIASA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI