Wizara ya nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira imewapiga faini ya milioni 5 Wananchi 9 wa kiwalani kila mmoja baada kuonekana kuwa wamevunja sheria ya Mazingira kwa kupeleka chemba za maji machafu kutoka majumbani kwao na kuingiza katika mfereji unaotoka uwanja wa ndege.
Wizara pia imevipiga faini viwanda viwili kikiwemo kiwanda cha A one, faini ya million 10 na steps entertainment inatakiwa kulipa million 7 kwa kosa la kuelekeza maji machafu kutoka kiwandani kuingia katika Mazingira bila kuwa na kibali cha serikali. Fedha zote jumla ya milioni 67 zimetakiwa kulipwa ndani ya siku saba.
ULIKOSA KAULI YA TUNDU LISSU BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI