Najua utakuwa ilisikia stori za mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anaichezea klabu ya Azam FC Didier Kavumbagu kuripotiwa kufungiwa na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutokana na kudaiwa kusaini timu mbili tofauti ndani ya Ligi ya Vietnam, stori zilienea sana lakini Kavumbagu kaweka ukweli wote Sports Extra ya Clouds FM.
“Ukweli sijafungiwa ila kuna matatizo ya mikataba yalinikuta Vietnam timu iliyokuwa imeeniita nilikuta imemsajili mbrazil kutokana na mimi kuchelewa kufika, lakini nilitafutiwa timu nyingine nikafuzu majaribio na kusaini mkataba baadae wakagombana na meneja wangu nikaenda timu nyingie FIFA wakasema mchezaji mmoja hawezi saini mkataba timu mbili”
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2