Bado headlines za wekundu wa Msimbazi Simba kutaka kununuliwa na bilionea wa 21 Afrika Mohammed Dewji zinatawala katika vichwa vya habari, mfanyabiashara na mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji katika mkutano mkuu na wanachama uliofanyika leo August 6 Diamond Jubilee ameomba wanachama wa Yanga wamkodishie timu.
Manji ameomba apewe timu ya Yanga na nembo ya klabu hiyo huku majengo akisema yabaki kwao, asilimia 25 ya faida itaignia kwa klabu lakini gharama za uendeshwaji wa timu zote zitakuwa chini yake katika kipindi cha miaka yote 10 aliyoomba.
“Nipeni timu na nembo halafu majengo yabakie kwenu ikitokea hasara nitalipa mimi na ikipatikana faida asilimia 25 itakuja kwa klabu, nipeni uhuru na timu yenu mimi najua namna ya kuiendesha ikashindana na Azam FC na gharama za uendeshaji nitalipa pia, jumanne naunda kampuni itakayokuja kupangisha timu ya Yanga kwa miaka 10”
“Katika kipindi cha miaka 10 ikipatikana faida asilimia 25 itakwenda kwa klabu na wanachama na asilimia 75 kwangu, kama itakuwa ni hasara basi itakuwa ni hasara yangu hakuna hasara kwa klabu wala wanachama, tayari nimetuma ombi kwa bodi ya wadhamini waongee na nyinyi na kama tutakubaliana tutaingia mkataba”
ALL GOALS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1