Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja habari zilizoandikwa ni hii habari kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Miamala ya simu bei mpya balaa’
#NIPASHE Yadaiwa kampuni za simu zimepandisha mara dufu gharama za kutuma, kupokea fedha bila kutoa taarifa kwa umma pic.twitter.com/PKtaQE6eTn
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
Wakati Serikali ikisema uanzishaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwenye miamala ya simu na benki haitawahusu wateja, kampeni za simu zimepandisha mara dufu gharama za kutuma na kupokea fedha.
Tofauti na benki ambazo zinatoa matangazo kwa umma juu ya kupandisha gharama miamala na huduma zake kabla ya mwaka wa bajeti wa 2016/17 kuanza, kampuni za simu zimepandisha gharama bila kutoa taarifa kwa umma.
Kutokana na tangazo la benki la hizo, tangu julai mosi watumiaji wa huduma za kibenki walitarajiwa kuanza kukatwa asilimia 18 ya kodi ya VAT katika kila muamala wanaoufanya ambazo ni kati ya sh. 152.50 katika kila mapato ya sh. 1000 yanatozwa na benki, mteja anapofanya muamala.
Baada ya tamko hilo la benki, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alipinga hatua ya benki hizo na huku Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Benno Ndulu akisema kwamba benki ziko sahihi kupandisha gharama hizo.
Kwa mujibu wa Kidata , BOT zinapaswa kusimamia benki ili zisiongeze gharama hizo na mamlaka ya mawasiliano (TCRA), kubana kampuni za simu zisipandishe gharama.
Tangu juma lililopita, wateja wa kampuni za simu walianza kuonja chungu ya VAT baada ya kodi, baada ya kuanza kushuhudia wakikatwa fedha kiwango kikubwa zaidi ya ilivyokuwa awali.
Katika mazungumzo na gazeti la Nipashe na watoa huduma za fedha za mitandao ya simu, walisema hata wao walianza kupata malalamiko kutoka kwa wateja kwamba wanakatwa fedha nyingi kuliko ilivyokua mwanzo.
Mmoja wa wateja aliyejitambulisha kwa jina moja la Henry alilielezea Nipashe kuwa alikua anatoa sh. 625,000 kutoka mtandao wa vodacom kwenda Tigo akakatwa sh. 10,500……>>>‘Kwa kawaida ilitakiwa nikatwe sh 7,500 lakini siku ile nilishangaa makato yameongeeka’
Mteja mwingine Hassan Jamal alisema alitumiwa sh. 900,000 kwenye mtandaowa Tigo na alivyotoa alikatwa sh. 8000
Source: Nipashe
#MTANZANIA Mwenge wa uhuru wazua balaa Mwanza, walimu watakiwa kukesha wakiushangilia, Chama cha walimu chapinga pic.twitter.com/pgGnxXNUic
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MTANZANIA BAVICHA wasema wameanza maandalizi ya Operesheni UKUTA, wapinga maagizo ya ma-RC kwa vyombo vya ulinzi pic.twitter.com/AeGdPnfqQV
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MTANZANIA Mkazi Chamwino adaiwa kumuua baba yake kwa kumpiga teke mbavuni, sababu zikitajwa kuwa ni kugombea redio pic.twitter.com/hL26QtgPQ3
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MTANZANIA Muhimbili inakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni inayodaiwa na wazabuni yanayokadiriwa kufikia bil 13 pic.twitter.com/BPzvYtw9e3
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MTANZANIA Mke wa bilionea Erasto Msuya amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya dada wa Msuya, Aneth Msuya pic.twitter.com/ECi5mCsovr
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MTANZANIA DC K'ndoni amepiga marufuku wanaoendelea kufanya siasa ktk soko la mwenge kwa vile muda wa siasa umepita. pic.twitter.com/LEggStBY0x
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#JamboLEO CCM yapuuza utafiti ulioainisha Watanzania kutoiamini Taasisi ya Rais na kudai watafiti wana lengo ovu pic.twitter.com/9oBRiR4e0K
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#JamboLEO Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema hupokea wastani wa wagonjwa 100 wanaofika kubadilisha damu kila siku pic.twitter.com/fcLuLO4LZb
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#JamboLEO UNICEF imebainisha kuwa Z'bar ina kiwango cha chini unyonyeshaji maziwa ya mama pekee miezi 6 ya kwanza pic.twitter.com/hp17wPy9TI
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MWANANCHI Watumishi wasainishwa saa 9 usiku mkesha wa Mwenge, CWT yataka watakaokwenda wadai posho 180,000 pic.twitter.com/sG9dT0iwiH
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#MWANANCHI Wenye majengo yanayopangishwa na kupata zaidi ya 500,000 kwa mwaka wametakiwa kujipanga kulipa kodi pic.twitter.com/xfWHLN4ZQd
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
#NIPASHE Mwl Mkuu shule ya Sekondari Mwendakulima, Kahama mbaroni kwa kuruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi shule pic.twitter.com/WK9CsL2iJb
— millardayo (@millardayo) August 8, 2016
UMEKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI AUGUST 08 2016 KUTOKA AYO TV?UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI