August 10 2016 majira ya jioni kumetokea ajali ya moto ambayo imesababisha kuteketea kwa jengo la Bar maarufu Carebean iliyopo Sinza White Inn, chanzo cha moto huo inasadikika ni itilafu ya umeme.
Kikosi cha zimamoto kimefika kwa ajili ya kuzima moto huo na mpaka millardayo.com inaondoka eneo la tukio hakuna mali iliyookolewa kutoka kwenye kwenye bar hiyo na hakuna aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto.
Akizungumza na millardyo.com na Ayo TV, Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala, Chacha Mchaka amesama….>>>’changamoto ambazo tumezipata ni foleni, tumechelewa kufika na pia visima vya maji viko mbali zaidi ndio maana vikosi vyetu vimeondoka maeneo mengine kuchukua maji lakini tungekuwa na visima hapa karibu tungekuwa tushamaliza zoezi hili’.