Mtu wangu kama unakumbuka mwezi July 2016 tulimsikia Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga alituelezea kuhusu watanzania ambao wamekamatwa wakienda kujiunga na kikundi cha ugaidi cha Al shababu Somalia.
Leo August 11 2016 Waziri Mahiga alikutana na waandishi wa habari na wakawa wamemuuliza suala la kuwepo kwa watanzania waliojiunga na kikundi cha waasi cha AFD ambapo Waziri Mahiga amesema………
>>>’tulipokwenda kwenye kikao cha maziwa makuu kule Angola Rais Kabila mwenyewe akasema na ananitazama kama vile ananiambia mimi, anasema kule kuna watanzania, anasema pengine Serikali yenu haijui lakini kuna vijana wanajihusisha na kwamba mkuu wa kikundi kile alikamatwa hapa Tanzania’
ULIKOSA HII YA WATANZANIA KUUAWA NA WENGINE KUKAMATWA WAKIJIHUSISHA NA AL- SHABAAB? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI