Siku kadhaa zilizopita kulitokea jaribio la mapinduzi nchini Uturuki la kumpindua Rais wa nchi hiyo ambapo mitaa mbalimbali ilifungwa na baadhi ya wanajeshi ambao walitaka kupindua serikali hiyo.
Nchini Tanzania wiki hii zikawa zimesambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mmiliki wa shule za Feza anahusika kufadhili mapinduzi hayo na kuwa Serikali ya Uturuki imeiomba Serikali ya Tanzania kufungia shule za Feza nchini kuwa zinahusishwa na kufadhili mapinduzi ya nchi hiyo.
Leo August 11 2016 uongozi wa Shule za FEZA kupitia kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule, Habib Midraji amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa Shule hizo zitafungwa wakati wowote na kuwa shule hizo hazina uhusiano na Fethullah Gulen ambaye inadaiwa kuwa ndio mmiliki na pia Shule hizo si Mali ya serikali ya Uturuki na hazipokea misaada kutoka pande hizo mbili.
Aidha Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga amethibitisha kupokea barua kutoka ubalozi wa Uturuki kuhusu kufungia shule hizo za fedha ambapo amesema …..
>>>’tuhuma zimekuja kwamba hizi shule za fedha ni seheemu za makundi yanayoipinga Serikali hii na kwamba ndani ya hizi shule walimu wanaofundisha wanapenyeza itikadi ya kigaidi katika hizi shule, sasa ubalozi hapa unasema kati ya makampuni hayo kuna makampuni mengine amTanzania yanakusanya fedha kwa ajili ya kufadhili vikundi vya upinzani’
>>>’Serikali kabla haijatoa kibali kwa shirika lolote la elimu huwa inafanya upekuzi, ubalozi wa Uturuki wametuambia hawa waliopo hapa ni magaidi na sisi tunataka kupata ushahidi kamili’
ULIKOSA HUU MPANGO WA MWANZA KUJENGEWA DARAJA KAMA LA KIGAMBONI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI