Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 11 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka ITV…
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameyazungumza haya kwa vyuo
>>> ‘kuna kipindi ambacho pengine vyuo vilikuwa vinajisahau, mtu anaamua kuweka bango lake kuna chuo kumbe hajasajiliwa na sisi kama Serikali tunavikagua vyuo vyote na tunavyoona havina sifa tutaendelea kuvifungia kwasababu kimsingi wale wanafunzi wakimaliza hawawezi kupata ajira kwasababu wamemaliza katika vyuo ambavyo havitambuliki na Serikali….’
Habari kutoka Azam TV
>>> ‘Hii sio taarifa nzuri kwa sisi wafanyakazi wa hali halisi publishers tunaochapicha gazeti la Mseto lakini taarifa hii inapaswa kutazamwa kwamba ni taarifa kandamizi kama tunavyoiona inalalamikiwa na wadau, kwahiyo wanatumia sheria zilizo mbovu kukandamiza waandishi wa vyombo vya habari katika nchi kwasababu hawakutuambia tudhibitishe wangetuambia tudhibitishe hilo lingekuwa swala lingine…’ – Mwandishi wa gazeti la Mseto
Habari kutoka ITV
Eneo la Same mkoani Kilimanjaro kuwa kutajwa kuwa eneo la ukame na kusababishwa na uharibifu wa mazingira na kutokana na umasikini kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwa na athari kwa tabia ya nchi kutokana na wananchi kuharibu mazingira kupelekea kuwepo na tishio la njaa na uhaba wa maji.
Habari kutoka Star TV
Waziri wa Ardhi, nyumba na Makazi -Mhe William Lukuvi ametoa miezi mitatu kwa watu wanaomiliki hati zaidi ya elfu moja kuanza kuuza viwanja vyao tofauti na hivyo serikali itavitaifisha.
Habari kutoka ITV
Ziara ya Rais Magufuli Mwanza
>>> ‘Mkandarasi wa daraja eneo la Furahisha Mwanza atakiwa kumaliza ujenzi wa daraja hilo kabla ya December 25 2016‘ – Rais Magufuli
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA RAIS MAGUFULI ALIVYOINGILIA KATI MGOGORO WA WAMACHINGA NA MANISPAA JIJINI MWANZA? UNAWEZA KUITAZAMA NIMEKUWEKEA VIDEO HAPA CHINI