Hivi karibuni serikali kupitia baraza la Taifa la usalama barabarani Tanzania lilitangaza kuanzisha mkakati wa miezi sita unaolenga kukabiliana na ajali za barabarani nchini kwa muda mfupi kuanzia August 2016 hadi February 2017 lengo likiwa kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa ambayo hupelekea ajali za barabarani kuongezeka.
Ayo TV imemtafuta Kamanda mkuu wa Polisi usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga ambaye ametupa takwimu ya watu kukamatwa kwa makosa ya usalama barabarani.
‘Tumeanza kukamata watu mbalimbali wanaofanya makosa mfano leo pekee tumeshawakamata madereve wavunja sheria zaidi ya 30 ambao wote tutawafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani‘- Mohamed Mpinga
‘Mkakati wetu unakwenda vizuri na nisisitizetu kuwa suala la kuomba msamaha kwa kuvunja sheria za barabarani hatutakuwa na msamaha bali ni kuwapeleka mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake‘ –Mohamed Mpinga
ULIKOSA YA UKIKAMATWA NA TRAFIKI KWA KUPITA BRT