Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya August 20 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Miujiza mihogo mibichi, Mbata kwa wanaume’
#NIPASHE Mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa na akinamama Dar vyatajwa kuwasaidia maelfu kulinda heshima ya ndoa zao pic.twitter.com/Tq1BRORON0
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
Gazeti la Nipashe limeripoti kuwa uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebainisha kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na akina mama jiini Dar es salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zink na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambatana cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.
Mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es salaam aliiambia Nipashe……..>>>’Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya akina baba, vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarishha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenza wao‘
Ofisa utafiti wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitishwa kitaalam kuwa husaidia kuimarisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayotokana hasa na Zinc.
Alisema kwa sababu hiyo ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es salaam na kwengineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa akina mama.
SOURCE: NIPASHE
#MWANANCHI PAC yabaini madudu wizara ya Elimu ktk uandaaji wa harambee Marekani, bil 1.2 zilitumika bila mafanikio pic.twitter.com/NSb3q8PZsv
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MWANANCHI Ishara ya Maalim Seif kwa Rais Shein kusalimiana yazusha mapya CCM yataka asishirikishwe hafla za kitaifa pic.twitter.com/idyA8Q1cPe
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#NIPASHE Mfanyabiashara na mmiliki shule ya sekondari Merinyo Moshi amejiua kwa kujimwagia petroli na kujiwasha moto pic.twitter.com/dtaGZunGiA
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#NIPASHE Mafanikio ya kuhamisha makao makuu Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja ni miongoni mwa siri 5 kuhamia Dodoma pic.twitter.com/2V30QlRzQm
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#NIPASHE TRA kuanza msako nyumba kwa nyumba kuhakiki gharama za upangishaji ili kutoza kodi ifikapo September 2016 pic.twitter.com/zWUqEM0bIt
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MWANANCHI Hatua ya kuondolewa kwa aliyekuwa RC Arusha, Ntibenda baadhi ya wachambuzi wasema ni mikakati ya kisiasa pic.twitter.com/cZcH2A0ijk
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MWANANCHI Maambukizi mapya ya VVU Mbeya yamekuwa juu ya 9% na kusababisha kupunguza nguvu kazi ya Taifa pic.twitter.com/p8NDhS6y2F
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MTANZANIA Mahakama Kisutu yatupilia mbali pingamizi lilitolewa na Jamhuri la kumzuia wakili Kibatala kumtetea Lissu pic.twitter.com/EkHHJl6EiS
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MTANZANIA Mawaziri kutoa taarifa ya utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti kwa kila mwezi kupitia vyombo vya habari pic.twitter.com/cYWU80JymQ
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MTANZANIA Waziri Lukuvi afuta umiliki wa ardhi wa zaidi ya ekari 2188 zilizomilikiwa na raia wa uingereza Kagera pic.twitter.com/9TLMdx4Jwa
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#JamboLEO Bandari ya Dar es salaam kutumia bil 145 kwa ajili ya kufanyiwa maboresho pic.twitter.com/Uq3P95CgOs
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#HabariLEO Asasi za kiraia na kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 5000 hatihati kufutiwa usajili pic.twitter.com/UxZ9BYogXl
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#HabariLEO SUMATRA yasema hakuna usafiri utakaositishwa na inafuatilia kuhakikisha huduma inatolewa wakati wote. pic.twitter.com/dXZzX82AaF
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#HabariLEO Polisi Dar yabaini mbinu inayotumia na wahalifu kuingiza bidhaa za magendo kwa kutumia ng'ombe na punda pic.twitter.com/EU8dJIsrZV
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
#MAJIRA Mahakama Kisutu yatoa masharti ya dhamana washtakiwa wawili NIDA kwa kuwa mashtaka yao si ya kuhujumu uchumi pic.twitter.com/u7zhfyuxg5
— millardayo (@millardayo) August 20, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI AUGUST 20 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI